WAREHOUSE BAR
Warehouse Bar ni ukumbi wa kipekee wa wazi ulio katikati ya mji wa kisasa wa Dar es Salaam. Ni Vinara na wababe na wazoefu wa kipekee katika burudani Tanzania.Burudani ya kiwango cha kukata na shoka, Customer Care ya hali ya juu, na huduma bora.Wanapatikana masaki.
Pia hutoa huduma ya ukumbi kwa ajili ya sherehe , hafla za kibinafsi, sherehe za kuzaliwa, hafla za kampuni, na maadhimisho maalum.
Muziki utapata wa ladha mchanganyiko mbalimbali unaokidhi matakwa tofauti ya wateja. Warehouse Bar huwaleta DJs maarufu na bendi za moja kwa moja, wakicheza aina za muziki kama Amapiano, Afrobeat, Bongo Flava, Hip-Hop, R&B na House. Iwe uko kwenye hali ya kukesha usiku kucha au kufurahia jioni tulivu na marafiki, muziki wa Warehouse Bar utakupa mazingira mazuri .
Kwa wale wanaotafuta utulivu wa kipekee, kuna sehemu ya VIP inatoa meza za binafsi, huduma ya vinywaji, na wafanyakazi maalum kuhakikisha usiku wako unakuwa bomba.
Vinywaji Vya aina zote vinapatikana Warehouse Bar . Kaunta imejaa aina mbalimbali za vinywaji, kuanzia local bia hadi vile vya kimataifa vinavyotamba kama martel,Johny walker na nyinginezo nyingi.
Warehouse bar utapata kokteli za kupendeza na za kiwango cha juu, mvinyo, bia, pamoja na non alcoholic drinks kama soda aina zote.
Mimi binafsi nimekuwa mteja wa hapa kwa muda mrefu sasa, na ingawa siendi kila mwisho wa wiki (kuna sehemu nyingi ambazo pia ninahitaji kutembelea na kukutana na watu), hii ni sehemu ambayo daima iko juu kwenye orodha yangu ya sehemu zinazotoa burudani ya nguvu jijini Dar es Salaam. Ikiwa hujawahi kufika warehouse baa , basi pangilia muda wako ukatembelee msimu huu wa sikukuu.
WAREHOUSE BAR LOCATION
If you want to read more reviews on bars in Dar Es Salaam, then CLICK HERE.
If you want to support our project, why not follow us on LinkedIn (CLICK HERE) or Facebook (CLICK HERE) – or why not both?